yanga yatua tanga kimya kimya

Baada ya kutoa dozi kwa Kagera Sugar, kikosi cha Yanga tayari kimetua jijini Tanga kwa ajili ya kutafuta pointi tatu nyingine kwenye mchezo wa ligi kuu utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani. Mkuu wa kitengo cha habari na mawasililiano cha klabu ya Yanga Jerry Muro amesema, vita yao ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu inaendelea kwa kuwa kila mchezo kwao ni fainali. “Kikosi chetu tayari kimeshawasili jijini Tanga, vijana wameingia Tanga pasipo watu kujua kama wameingia watu walistukia tu kikosi kipo mkoani Tanga,” alisema Muro. Muro ametamba kuwa kikosi chao kitaibuka na ushindi kwenye mchezo huo licha ya Mgambo kuwatandika watani wao wa jadi kwa goli mbili bila majibu kwenye mechi yao iliyopita. “Wasitufananishe sisi na Simba, Simba siyo mwenzetu sisi ni wa kimataifa zaidi, wao ni wa mchangani sasa huwezi ukalinganisha timu ya mchangani na timu ya kimataifa. Wao kufungwa ilikuwa ni desturi, sisi kwetu ushindi ni jadi yetu hata ukiangalia ‘trend’ (mwenendo) kwenye ligi nani ameshinda michezo mingi, nani yuko wapi anafanya nini, utaweza kututofautisha na wao,” Muro alitamba. Kwa upande wa kocha wa Mgambo JKT Bakari Shime amesema licha ya kuwa na mechi tatu ngumu ndani ya siku saba haitawazuia wao kufanya vizuri kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga. “Tumekuwa na mechi tatu ngumu mfululizo ndani ya siku saba, tulicheza na Mbeya City, baada ya hapo tumecheza na Simba na mchezo wetu unaofuata tutacheza na Yanga. Lakini hiyo haituzuii sisi kufanya vizuri,” alisema Shime. Kesho Mgambo JKT watakuwa wenyeji wa Yanga kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara, Mgambo walishinda mchezo wao wa mwisho kwa goli 2-0 dhidi ya Simba, wakati Yanga wenyewe walishinda 2-1 mbele ya Kagera Sugar.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: