STEVEN GERRARD NA KIATU CHA MECHI YA 700 LIVERPOOL

KIUNGO Steven Gerrard amekuwa mchezaji wa tatu wa Liverpool kutimiza mechi 700 kihistoria baada ya kuichezea timu hiyo jana ikishinda 1-0 dhidi ya Bolton katika mechi ya marudio Raundi ya Nne ya Kombe la FA. Nahodha huyo wa Liverpool, alirejeshwa kwenye kikosi cha kwanza na kocha Brendan Rodgers, na kuingia kwenye orodha ya Ian Callaghan na Jamie Carragher walioichezea pia mechi 700 klabu hiyo. Gerrard, ambaye maisha yae yote amecheza Liverpool tu, alifurahia mafanikio yake hayo kwa kuvaa kiatu maalum kilichoandikwa 700 nyuma pamoja na majina ya mabinti zake, Lilly na Lexie.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: