Serikali imeaswa kuharakisha kumalizia ujenzi wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha songwe jijini mbeya ili kuchochea ukuaji wa sekta ya utalii kanda ya nyanda za juu kusini yenye utajiri wa vivutio vya vingi vya utalii ambavyo haviajatangazwa na kujulikana vyakutosha.
Rai hiyo imetolewa na meneja wa kiwanja cha ndege cha kimataifa cha songwe bwana valentine kadeha wakati akizungumza na waandishiwa habari ofisini kwake na kueleza kuwa baada ya serikali kuanza zoezi la upanuzi wa kiwanja hicho mashirika ya ndege yameongezeka kutumia kiwanja hicho na kuongeza idadi ya abiria wanaosafiri kupitia kiwanja cha songwe jijini mbeya kutoka.
Abiria 3,000 hadi 12,000 kwa mwezi hali inayotia matumaini ya kuchochea ukuaji wa shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo sekta ya utalii.
Vivutio hivyo vya utalii vimekuwa vyanzo vizuri vya mapato katika maeneo vilipo huku baadhi yake vikitumika kama matambiko ya wenyeji hali ambayo inaweza kufanya vivutio hivyo kutumika pia kutangaza utamaduni wa maeneo husika kama anavyoeleza bwana adam elia mwenyekiti wa kitongoji cha mapandana.
Baadhi ya vivutio vya utalii vinavyopatikana katika ukanda wa nyanda za juu kusini ni pamoja na kimondo cha mbozi kilichogunduliwa miaka ya 1930 wilayani mbozi daraja la mungu huko kiwira mkoani mbeya hifadhi za taifa za ruaha na kitulo katika mikoa ya mbeya iringa na njombe maporomoko ya maji pamoja na kijungu kinachopatikana katika mto kiwira ambapo baadhi ya wadau wameiomba serikali kuboresha miundombinu ili kuwezesha watalii kufika katika vivutio hivyo.
Home
Uncategories
SERIKALI IMEASWA KUARAKISHA KUMALIZIKA KWA UJENZI WA UWANJA WA KIMATAIFA WA SONGWE
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment