Mbeya
POLISI Mkoani Mbeya, imetoa ufafanuzi kufuatia vurugu zilizofanywa na wananchi wa Mji mdogo wa Mbalizi na baadhi ya askari wa jeshi la wananchi kikosi cha 44KJ cha Mbalizi,
na barnabas njenjema mbeya
ambapo vurugu hizo zilisababisha kifo cha askari mmoja.
Aidha imeelezwa kuwa , vurugu hizo hazikusababishwa na ugomvi wa kimapenzi kama ulivyoelezwa na kuenezwa na baadhi ya watu bali ni ugomvi ambao uliwahusisha baadhi ya vijana raia na wanajeshi wa kikosi cha Mbalizi 44KJ baada ya mwanajeshi mmoja aliyepanga ulaiyani kuibiwa mali zake.
Akimtaja askari huyo aliyeuawa katika vurugu hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, amesema ni marehemu mwenye namba FT 1096619 Mwaka Ahadi kutoka kikosi namba 825 cha JKT Mtabila kilichopo Mkoani Kigoma.
Aidha, amesema kuwa askari huyo alipoteza maisha wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Jeshi ya Mbalizi kikosi cha 44KJ.
Akielezea sababu za vurugu hizo, Msangi amesema, viashiria vya kutokea kwa vurugu hizo, vilianza kutokea siku ya Jumanne ya tarehe 3 mwezi February, 2015 baada ya kukamatwa kwa vijana nane na kufikishwa katika kituo cha Polisi cha Wilaya ya kipolisi ya Mbalizi kwa tuhuma za wizi wa radio na televisheni.
Amesema, kwa mujibu wa taarifa hizo, inasemekana kwamba katika msako huo vijana nane walikamatwa kati ya tisa na kufikishwa katika kituo cha polisi.
Amesema, hivyo wananchi walipowaona wanajeshi kwenye eneo lao walianzisha vurugu zilizoambatana na uvunjifu wa amani .
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment