MSHAMBULIAJI wa klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mrisho Ngassa, amejutia uamuzi wake wa kukataa kujiunga na El Merreikh ya Sudan akisema kuwa yalikuwa ni mapenzi yake makubwa kuichezea Yanga.
Akiongea na Shaffihdauda.combaada ya mchezo wa jana alipoibuka shujaa kwa kuifungia Yanga bao 2-0 dhidi ya Mtibwa Sugar, Ngassa alisema kuwa baada ya kugundua alifanya makosa makubwa kuwagomea Simba na Azam FC ambao ndio walitaka kumpeleka El Merreikh, alipofunga mabao hayo alilazimika kuwaomba msamaha mashabiki kwa uamuzi ambao sasa anaujutia.
“Nilifanya makosa kutokwenda El Merreikh ndio maana hata leo nilipofunga magoli ilibidi niombe msamaha kwa sababu Simba na Azam walitaka kunipeleka El Merreikh, Nilifanya kama kuwakosea na kwasababu nilikuwa naipenda Yanga ilibidi niichezee” Amesema Ngassa kwa hari ya uchungu ajijuta kosa alilofanya katika maisha yake la kukataa kwenda kucheza mpira wa kulipwa nchini Sudan.
Katika msimu wa 2013/2014 Ngassa alijiunga na Yanga akitokea Simba alikokuwa akicheza kwa mkopo akiwa ni mali ya Azam FC, Katika uamisho huo TFF iliamuru awalipe Simba kiasi cha Tsh. Milioni 30 kama pesa ambayo walimsajilia kutoka Azam FC pamoja na Tsh. Milioni 15 kama fidia baada ya kugundulika alikuwa amesajiliwa timu mbili zaidi ya hapo TFF ilikuwa imepanga kumfungia endapo asingelipa deni hilo
Home
Uncategories
NGASSA AJUTA KUWATOSA EL MERREIKH, AOMBA MSAMAHA MASHABIKI WA SIMBA, ADAI YANGA WAMEMGEUKA
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment