Hatimaye Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Kikwete ametangaza rasmi kufuta ada katika shule za sekondari zote za umma nchini Tanzania. Hatua inafuatia ahadi aliyoitoa Agosti Mwaka jana chuo kikuu cha Mzumbe Morogoro. Aidha, akizindua Sera mpya ya Elimu na Mafunzo 2014 katika Shule ya Sekondari ya Majani ya Chai, Kipawa jijini Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alitangaza kufutwa kwa ada ya sekondari, kuanzia mwakani 2016. Kutokana na uamuzi wa Rais Kikwete Bajeti itakayojadiliwa Mei mwaka huu, itatakiwa kuwa na fungu la kulipa gharama ambazo wananchi wamekuwa wakitoa kwa watoto wao wanaosoma elimu ya sekondari katika shule za Serikali nchi nzima. Kabla ya kufutwa ada, wanafunzi wamekuwa wakilipa kiasi cha shilingi elfu ishirini (20,000) kwa shule za kutwa na wale wanaosoma shule za bweni shilingi elfu sabini (70,000). Wakiongea na Mwandishi wa Habari wa Hivisasa baadhi ya wazazi wanao somesha watoto wao katika shule mbalimbali za sekondari jijini Dares salaam wamempongeza Rais Kikwete kwa uamuzi wake wa Kufuta ada katika shule za Sekondari ili mwanafunzi aweze kupata elimu ya upili bure. Hata hivyo,wazazi wameiomba serikali kuhakikiksha kuwa wanadhibiti michango mashuleni kwa sababu kumekuwa na mazoea ya walimu kuhamishia ada kwenye michango suala linalopelekea kuto onekana unafuu wa kufutwa ada hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: