EWURA yashusha bei za umeme, kuanza rasmi machi 2015

Dar es salaam, mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inatarajia kushusha bei za umeme kuanzia machi mosi mwaka 2015. Hatua hiyo inafuatia kushuka bei za mafuta katika soko la dunia. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, alisema kushuka kwa gharama hizo kunatokana na mabadiliko ya gharama za shirika la Umeme (Tanesco), kutokana na mabadiliko katika bei ya mafuta, thamani ya fedha na mfumuko wa bei. Bei mpya zitakuwa kama ifutavyo: Kwa bei hiyo ya watumiaji wa kawaida, umeme wa Sh 10,000 kwa bei ya zamani mtumiaji alikuwa akipata uniti 32.67, sasa kwa bei hiyo atapata uniti 33.5, ambayo ni ongezeko la uniti 0.88. Wateja waliounganishwa katika msongo wa kati wa umeme, bei ya umeme itashuka kutoka Sh 163 kwa uniti hadi Sh 159 kwa uniti sawa na punguzo la Shilingi nne kwa uniti moja. Ngamlagosi alisema kwa wateja waliounganishwa katika msongo mkubwa wa umeme, vikiwemo viwanda, migodi na Zanzibar bei ya umeme itashuka kutoka Sh 159 kwa uniti hadi Sh 156 kwa uniti sawa na punguzo la Shilingi tatu kwa uniti. Kwa wateja wa majumbani wenye matumizi madogo ya wastani wa uniti 75 kwa mwezi, bei ya umeme haitabadilika kutokana na kwamba kundi hilo bei yake ni chini kutokana na gharama zake kuchangiwa na kundi la wateja wakubwa wa majumbani. Katika hatua nyingine amesisitiza kuwa kulingana na agizo hilo na kipengele cha saba cha kanuni za kupanga bei ya Umeme, bei za umeme zinatakiwa kurekebishwa kila baada ya miezi mitatu, kutokana na mabadiliko ya bei ya mafuta, thamani ya shilingi ya Tanzania na mfumko wa bei
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: