Bingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara timu ya Azam FC leo itamaliza ziara yake huko Lubumbashi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa kucheza mchezo wa mwisho na klabu ya Don Bosco
Mchezo utapigwa katika uwanja unaotumiwa na wenyeji wao timu ya TP Mazembe majira ya jioni hii na kufuatiwa na mechi nyingine kati ya Mabingwa wa DRC TP Mazembe dhidi ya Mabingwa wa Zambia ZESCO United.
Ziara ya Azam ni kwa ajili ya maandalizi ya michuano ya klabu bigwa barani Afrika raundi ya awali ambapo Azam atacheza na El-Merreikh ya Sudan, pamoja na ligi kuu ya Tanzania inayoendelea .
Azam walianza ziara yao kwa kupoteza mchezo mbele ya wenyeji TP Mazembe kwa kichapo cha bao 1-0.
Kisha wakakubali suluhu ya mabao 2-2 dhidi ya mabigwa wa Zambia ZESCO katika mchezo wao wa pili.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment