Zaidi ya asilimia 80 ya watu wanaogundulika kuugua ugonjwa wa saratani hufariki Dunia ikiwa ni kinyume na viwango vilivyowekwa na shirika la afya Duniani (WHO) ambapo asilimia 20 ya wagonjwa hao hupoteza maisha kama ilivyo katika nchi zilizoendelea.
Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa afya na Ustawi wa Jamii kufuatia kuelekea kwa maadhimisho ya siku ya Saratani Duniani hapo kesho ambapo amesema kuwa kwa hapa nchini idadi ya wagonjwa wapaya wa Saratani kwa kila mwaka ni zaidi ya 34,000 huku asilimia 10 ndio wanaofanikiwa kufika hospitalini kwa ajili ya matibabu, wakati huohuo asilimia 80 hufika wakiwa katika hatua za mwisho ya ugonjwa huo hali inayopunguza uwezekano wa kupona.
Aidha Dokta Rashid amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara ili kuondokana na tatizo la vifo vya saratani.
Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya kansa Hosipitali ya Ocean Road Dokta Diwani Msemo ameeleza kuwa kuongezeka kwa magonjwa ya saratani kunachangiwa na mabadiliko ya mfumo wa maisha huku akibainisha kuwa taasisi hiyo ina mpango wa kuingiza mitaala ya magonjwa ya saratani katika vyuo vya afya na kutoa elimu kwa watumishi wa afya kwenye hosipitali mbalimbali ili waweze kuvitambua mapema viashiria vya magonjwa hayo.
Maadhimisho ya siku ya saratani Duniani kwa mwaka huu yamebeba kauli mbiu isemayo udhibiti wa saratani uko ndani ya uwezo wetu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment