YAYA TOURE MWANASOKA BORA WA AFRIKA KWA MIAKA MINNE MFULULIZO

Kiungo mchezeshaji wa Manchester City, Yaya Toure ameibuka na kushinda tuzo ya mchezaji bora Afrika kwa mwaka 2014. Ushindi huo wa Toure unamfanya awe amechukua tuzo hiyo mara nne mfululizo. Toure, 31, ameibuka mshindi katika sherehe za tuzo hiyo zilizofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Lagos Nigeria. Raia huyo wa Ivory Coast amewashinda mshambuliaji wa Borussia Dortimund raia wa Gabon, Pierre-Emerick Aubameyang na kipa wa Nigeria Vincent Enyeama. Toure ameingoza Man City kubeba ubingwa wa England huku yeye akiwa amepachika mabao 20 na kuwa kiungo mwenye mabao mengi zaidi England.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: