Wanafunzi 29770 wafeli mtihani kidato cha pili

Matokeo ya kidato cha pili yametangazwa jana na Baraza la mitihani ya la Tanzania ambapo jumla ya wanafunzi 29770 wamepata alama za chini hivyo basi watashindwa kuendelea na masomo ya kidato cha tatu mwaka huu wa 2015.
Kwa mujibu wa Katibu mtendaji wa Baraza la mitihani la Tanzania (NECTA) Dk. Charles Msonde amesema kwa ujumla ufaulu umeongezeka kwa asilimia 3.32 ambapo masomo ya Sayansi, kilimo, Hisabati na Biashara wanafunzi wamefaulu chini ya aslimia 50.
Katika hatua nyingine alisema wanafunzi 375434 sawa na asilimia 92.66 wafaulu kuendelea na masomo ya kidato cha tatu kwa mwaka wa masomo 2014.
Ameongeza kuwa Masomo wanafunzi waliofaulu vizuri ni uraia, Historia, Kiswahili na kiingereza kwa asilimia 84 na kwa upande wa masomo ya Jiografia, Utunzaji hesabu ufaulu ni asilimia 50 hadi 70.
Mtihani wa kidato cha Pili kwa mwaka 2014 ni wa kwanza kusimamiwa na Necta ambapo miaka iliyopita ulikuwa unasimamiwa na idara ya ukaguzi kuanzia mwaka 1999.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: