VIJANA WATATU WA CHADEMA WALIOTEMBEA KWA MIGUU TOKA GEITA HADI DAR WAACHIWA KWA DHAMANA

i wish you happy chrismass and happy new year


Kamanda wa Polisi kanda ya Kinondoni Camilius Wambura alisema kuwa vijana watatu waliotoka Geita kuja Dar kwa lengo na kuonana na Rais na kukaidi amri ya kusitisha safari yao,wako nje kwa dhamana.

Kauli ya Wambura inatokana na vijana wa tatu kutoka Geita kutembea kwa miguu hadi Dar es salaam ili kuonana na Rais na kumweleza kero zao,ambapo walikamatwa baada ya kukaidi agizo la kusitisha safari yao.

Wambura alisema kinachofanyika kwa sasa ni taratibu za kusheria ikiwemo kufanyika kwa upelelezi na ukikamilika watawasiliana na mwanasheria wa Serikali kufahamu hatua gani inafuata.

Katibu mkuu wa Chadema Wilbroad Slaa alithibitisha mawakili wa chama hicho walikwenda kuwatoa vijana hao kwa maandishi na wamechukua jukumu la kuwasimamia mahakamani iwapo watashtakiwa.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: