UNYAMA..!! AMUUA MDAI WAKE KWA KUKERWA KUDAIWA SH 80,000 HUKO MKOANI MARA

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..



Kamanda wa Polisi mkoani Mara , Philipo Kalangi

MWANAMKE Caseline Mzee (75) mkazi wa kijiji cha Guta wilayani Bunda, mkoani Mara, ameuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kunyongwa na kisha mwili wake kutupwa ndani ya mto, ukiwa umefungiwa mawe mazito ili usielee. 

Mwanamume anayedaiwa kufanya mauaji hayo ametambuliwa kwa jina la Malaki Malongo (56) mkazi wa kijiji hicho, ambaye inadaiwa alimuua kinyama mwanamke huyo baada ya kudaiwa Sh 80,000, zilizotokana na huyo mama kumtibu mke wake ugonjwa wa kifafa.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara , Philpo Kalangi, alithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo lililotokea Desemba 31 mwaka jana saa 2:00 usiku katika kijiji cha Guta, ambapo mwili wa marehemu ulipatikana juzi ndani ya mto huo ukiwa umeharibika vibaya.

Kamanda Kalangi alisema chanzo cha mtuhumiwa huyo kumuua mwanamke huyo ni pale alipodaiwa Sh 80,000 ambazo ulikuwa ujira wake baada ya kumtibu mke wake ugonjwa wa kifafa.

Alisema mwanamke huyo alikuwa akiishi nyumbani kwa mwanamume kwa kipindi kirefu baada ya kutoka wilayani Serengeti, ambapo alitumia fursa hiyo kumtibu mke wa mwenyeji wake ugonjwa wa kifafa kwa makubaliano ya kulipwa Sh 80,000.

Alisema siku ya tukio mwanamume huyo alifika nyumbani hapo akiwa amelewa pombe na ndipo alipoingia ndani na kuanza kumshambulia kwa kipigo mwanamke huyo, huku akimwambia kwamba ni kwa nini amekuwa akimdai hizo fedha mara kwa mara.

Binti wa mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 13 aliyeshuhudia mauaji hayo, alisema baba yake alimpiga na kitu kizito kichwani mwanamke huyo na kisha akamnyonga hadi akakata roho.


Alisema baada ya mauaji hayo, baba yake alichukua mwili wa marehemu na kuuweka kwenye gunia la sandarusi na kisha akamlazimisha mke wake ili amsaidie kuubeba na kwamba walikwenda kuutupa ndani ya mto Nyandago ulioko mita 450 kutoka nyumbani kwao.

“Alimpiga na kitu kizito kichwani na kumnyonga shingo akitumia mikono, huyo mama alilia na kutoa sauti mara nne na kisha akanyamaza kabisa…..baba alichukuwa gunia na kuuweka mwili wa marehemu na kuufunga na ndipo akamlazimisha mama amsaidie kuubeba wakaenda kuutupa kwenye mto Nyandago,” alisema.

Binti huyo alisema baba yake wakati akifanya mauaji hayo, alimtishia kwamba kamwe asithubutu kumwambia mtu yeyote juu ya tukio hilo na kwamba kama atatoa siri hiyo atamuua kama alivyomuua mwanamke huyo.

“Aliniambia nikimwambia mtu yeyote na mimi ataniua kama alivyomua, nilinyamaza hadi juzi ndipo tukasikia yowe kwenye eneo la tukio na baba naye akaenda huko na ndipo wananchi wakamkamata na kuita polisi,” alisema.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: