Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..
Kila kukicha wizi huwa unakuja na mbinu mpya, Bongo zimezoeleka na kuvunjiwa milango, madirisha, kukatiwa nyavu na nyinginezo, kutoka Guizhou China kuna hii ya mbinu ya spiderman.
Jamaa alipanda jengo la ghorofa akitambaa kwa style ya spiderman, bahati mbaya yake akakutwa na askari kabla ya kufanya uhalifu wowote, wakaanza kumbembeleza ashuke, zoezi ambalo lilichukua zaidi ya saa moja ambapo huenda jamaa alikuwa na hofu juu ya hukumu atakayokutana nayo baada kukamatwa na askari hao.
Jitihada za kumbembeleza jamaa ashuke zilichukua muda lakini hatimaye akashuka, Polisi walimkamata na kuondoka naye.
China ni moja ya nchi ambazo kwa hatia ya makosa kama hayo hukumu yake ni kifo.
0 comments:
Post a Comment