Ukatili wa Kutisha!! JAMAA AMLIPUA KWA PETROL MKE WAKE KISA KWANINI AMEKATAA KUPASHA MOTO CHAKULA

Matuko ya kupiga na kunyanyaswa wanawake bado yameendelea kuchukua nafasi katika nchi malimbali za Afrika. Tumekuwa tukiona ripoti mbalimbali za matukio mabaya ya unyanyasaji, kutoka Kenya mwanaume mmoja amefunguliwa mashtaka baada ya jaribio la kutaka kumuua mke wake kwa madai alishindwa kumpatia chakula cha moto. Mwanaume huyo Peter Muthii alimmwagia mkewe petrol akiwa amelala, akawasha moto na kumfungia ndani ambapo muda mfupi baadaye majirani walikuja kumwokoa na kumkimbiza hospitali. Kisa cha tukio hilo kimetajwa kuwa ni baada ya mwanaume huyo kurudi nyumbani usiku na kumtaka mkewe kumpashia chakula lakini mkewe alimwambia apashe mwenyewe kitendo kilichomkwaza, akaamua kumlipua kwa kutumia petrol iliyokua chini ya kitanda chao
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: