UCHACHE VYOO SOKO LA FERI: WAVUVI, WATEJA WAJISAIDIA BAHARINI

Zaidi ya wavuvi 400 katika soko la samaki feri jijini Dar es Salaam wapo hatarini kukumbwa na magonjwa ya milipuko kutokana na kukosa vyoo kwa zaidi ya miaka 10. Hatari ya kuibuka kwa magonjwa katika eneo hilo inatokana na idadi kubwa ya wavuvi na wafanyabiashara kujisaidia haja ndogo na kubwa pembezoni mwa fukwe za eneo hilo huku maji hayo yakitumika kusafishia samaki. Akizungumza na Mwandishi wa HIVISASA baada ya kutembelea eneo la wavuvi Mwenyekiti wa wavuvi kanda ya nane Yahya Mohamed Masoud amesema kukosa huduma ya choo kwao limekuwa jambo la kawaida kwani wajisaidia kwenye fukwe hizo bila kujali athari za kiafya. Amesema licha ya kutoa taarifa za mara kwa mara katika uongozi wa soko na Halmashahuri ya Ilala lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa ili kukabiliana na tatizo hilo katika kipindi chote cha miaka 10 huku wakiendelea kutozwa ushuru wa mazingira. “Tumetelekezwa na serikali licha ya kuangaika kwenye ngazi zote za uongozi lakini tunaishia kuambiwa tusubiri hili eneo lote la feri lina vyoo viwili vya kulipia ambavyo haviwezi kuhudumia zaidi ya watu 1000 kwa siku mbali ya wateja wanaokuja kununua samaki”alisema Masoud.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: