SSERUNKUMA, MAGULI WAIPOTEZA NDANDA FC KWAO NANGWANDA SIJAONA

Kocha Goran Kopunovic ameanza Ligi Kuu Bara vizuri baada ya kuiwezesha Simba kushinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara.
Simba imeshinda mechi hiyo ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.
Vijana hao wa Msimbazi walifunga bao kila kipindi wakianza kupitia kwa Danny Sserunkuma aliyeonekana kufanya vizuri katika mechi hiyo.
Hata hivyo, Simba ilimaliza kipindi cha pili ikijilinda kutokana na wenyeji kucharuka na kushambulia sana.
Kipindi cha pili, Simba ilikianza vizuri na harakaharaka ilifanikiwa kupata bao la pili kupitia kwa Elius Maguli.
Huu ni ushindi wa pili kwa Simba tokea ilipoifunga Ruvu Shooting mwishoni mwa mwaka jana ukiwa ni ushindi pekee chini ya Patrick Phiri halafu ikatoka sare mechi sita na kupoteza moja dhidi ya Kagera Sugar.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: