SIMBA SC imegawana pointi na mabingwa watetezi, Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam baada ya kufungana bao 1-1. Matokeo hayo, yanaifanya Azam FC ifikishe pointi 21 baada ya mechi 11, wakati Simba SC sasa inakuwa na pointi 13. Mshambuliaji wa Simba SC, Mganda Emmanuel Okwi aliifungia timu yake bao la kuongoza, kabla ya kuzimia kipindi cha pili kufuatia kugongana na beki Aggrey Morris wa Azam na kukimbizwa hospitali ya taifa, Muhimbili. Okwi alitibiwa kwa dakika 10 kwenye zahanati ndogo iliyopo ndani ya Uwanja wa Taifa, lakini hakupata nafuu akakimbizwa Muhimbili.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: