MASHABIKI SIMBA WAMFUKUZA JUKWAANI STEVE AZAM, AANGUA KILIO

Mashabiki wa Simba, wamemfukuza jukwaani shabiki Steve Azam na kusababisha aangue kilio kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar. Steve ambaye alikuwa akijulikana kama Steve Yanga kabla ya kuamua kuhamia Azam FC, alikuwa amekaa kwenye jukwaa la Simba wakati timu yake ikitarajia kupambana na Simba. Hali hiyo ilionekana kuwaudhi mashabiki wa Simba ambao walimtaka ahamie jukwaa la Yanga lakini alishindwa kwa kuwa alishahama. Juhudi za kuwataka wamuache akae upande huo zilikwama, hivyo walinzi wa uwanja wakamshusha ndani uwanjani na kupewa hifadhi. Simba iko uwanjani ikipambana na Azam FC na hadi mapumziko inaongoza kwa bao 1-0 lililofungwa na Emmauel Okwi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: