Rais Kikwete ameatangaza Baraza jipya la Mawaziri katika mkutano na waandishi wa Habari ulioitishwa jioni hii ikulu jijini Dares salaam ambapo George Boniface Simbachawene ametuliwa kuwa waziri wa Nishati na Madini.
Akisoma mabadiliko hayo Katibu Mkuu Balozi Ombeni Sefue amesema kwamba baraza jipya la Mawaziri litaapishwa jioni hii Ikulu jijini Dares salaam. Simbachawene anachukua nafasi ya Prof Muhongo aliyejiuzulu wadhifa huo leo katika ofisi ya Wizara ya Nishati na Madini jijini Dares alaam.
Prof Muhongo amejiuzulu kuafuatia kutowajibika katika sakata la Akaunti y Tegeta Escrow lilipolekea upotevu wa mabilioni ya fedha ambazo ni za umma. Katika sakata hilo Waziri wa Ardhi Prof. Anna Tibaijuka pamoja na Mwanasheria mkuu wa serikali walijiuzulu.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment