NDEGE YA FASTJET YASHINDWA KUTUA JIJINI MBEYA

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!..


Ndege ya kampuni ya Fastjet imeshindwa kutua Mkoani Mbeya na kulazimika kurejea Jijini Dar es salaam kutokana na kuchafuka kwa hali ya hewa kulikoambatana na ukungu.

Ndege hiyo ilipaswa kutua saa 2 asubuhi katika uwanja wa ndege wa Songwe na kushindwa kutua na kulazimika kuzunguka hewani zaidi ya mara nbili ikitafuta mwelekeo.

Hali hiyo ilisababisha taharuki miongoni mwa abiria takribani 131 wakiwamo watoto kutokana na ndege kushindwa kutua.

Tuliogopa baada ya kuona imeanza kuzunguka zunguka hewani na tukaogopa kuwa huenda tukaanguka kwenye safu za milima ya Mbeya“alisema mmoja wa abiria.

Mratibu wa shughuli za ndege wa Shirika hilo Omary Idrisa alikiri hali ya hewa kuchagia ndege hiyo kushindwa kuruka.
Fastjet

WEKA MAONI YAKO HAPA

Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: