Kagera Sugar imepoteza mechi ya tatu mfululizo katika Ligi Kuu Bara baada ya kuchapwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wake wa 'nyumbani' wa CCM Kirumba mjini Mwanza.
Ndanda FC ndiyo waliokuwa wababe wa Kagera Sugar leo baada ya kuonyesha soka zuri na la kuvutia hasa katika kipindi cha pili.
Kocha wa Kagera Sugar, Jackson Mayanga amesema kuwa ma majeruhi wengi kumechangia wao kuendelea kuboronga kwenye dimba la Kirumba.
Kagera imekuwa ngangari kweli kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Kaitaba mjini Bukoba.
Mechi nyingine ilikuwa kati ya JKT Ruvu imemaliza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Mgambo katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar..
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment