Muuguzi wa zamani nchini Ujerumani amekubali kuwa ameua wagonjwa 30 katika hospitali ambako alifanya kazi kwa kuzidisha kipimo cha dawa ya ugonjwa wa moyo. Muuguzi huyo ambaye ana kesi mahakamani tangu septemba mwaka jana anadaiwa kusababisha mauaji ya watu 30 kwa kuwazidisha kipimo dawa suala analodai kuwa alikuwa anaboresha ujuzi wa kazi. Anadaiwa kuwa baada ya kuua wagonjwa watatu, alijaribu kuua watu wengine wawili katika kliniki ya Delmenhorst , karibu Bremen kaskazini ya nchi ya Ujerumani. Polisi wanachunguza zaidi ya tuhuma 100 ya vifo katika kliniki Delmenhorst . Hata hivyo Muuguzi, huyo aliyetambuliwa kama Niels H, alikuwa tayari amehukumiwa kifungo cha miaka saba na nusu gerezani mwaka 2008 kwa jaribio la mauaji.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: