Mikoa ya kusini iko hatarini kukosa huduma ya umeme kufutia kiwanda cha msimbati kinachotumika kuchakata gesi srdhi yake kumezwa na maji takribani mita mia moja na sita usawa wa bahari ambapo hadi sasa zimebakia mita 25 kufikia eneo lilipojengwa kiwanda hicho. Mikoa hiyo ni ya Lindi na Mtwara.
Kwa mujibu wa naibu waziri nishati na madini Bw. Charles kitwanga amesema kujaa maji katika kiwanda cha Msimbati kumetokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika nchi za Malawi na Msumbiji na hivyo kuleta madhara upande wa tanzania.
Ameongeza kuwa ameitisha kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama ambapo wanatarajia kutumia jeshi la majini na nchi kavu ili kusaidia kuzuia sehemu ya kiwanda iliyobaki isimezwe na maji.
Naye Muhandisi mkuu wa kiwanda hicho cha M and P Peter John akisema endapo ardhi hiyo itaendelea kumegwa wakati wowote watasitisha kazi ili kunusuru maisha ya watu na mali zinazohamishika.
Kwa upande mwingine dhoruba hiyo imetokea usiku wa tarehe 13 kuamkia tarehe 14 ambapo kipande cha ardhi chenye ukubwa wa mita miamoja na sita kiliweza kumezwa na maji
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment