Mgombea wa chama cha Patriotic Front Edga Lungu ameshinda uchaguzi wa urais nchini Zambia. Tume ya uchaguzi nchini humo imesema kuwa Lungu amepata asilimia 48 ya kura zilizopigwa.
Alikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea wa upinzani Bw. Hakainde Hichilema aliyepata asilimia 46. Katika kampeni zao wote walikuwa wameahidi kuboresha mifumo ya elimu na kubuni nafasi za ajira.
Uchaguzi huo umefanyika kufuatia kifo cha rais Michael Sata ambaye aliaga dunia mwezi Oktoba mwaka uliopita.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment