LIVE UPDATE SIMBA 1 VS AZAM 1: UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAM

Ligi tanzania bara inaendelea kutimua vumbi hii leo kwa michezo na viwanja kadhaa kuwaka moto hapa ni simba vs azam saa kumi kamili jion ni live update mtanange umeshaaanza kunako katika dimba la taifa ;; 19 emanuel okwi anaiandikia simba goli la kwanza Dk 42 Kapombe anapiga shuti lakini inazuiwa na kuwa kona inayochongwa na Kipre anapiga juuuuu Dk 36, Messi Singano anawatoka mabeki wa Azam na kutoa pais nzuri lakini wenzake wanashindwa kuwa makini. Dk 32, Kipre anatoa bonge la pasi kwa Kavumbagu, lakini anapiga shuti kuuubwa juu Dk 29, Azam FC inafanya shambulizi kali Tchetche anapiga shuti linaokolewa na mabeki wa Simba wakati likiwa limempita kipa Manyika. Dk 25, Simba wanafanya shambulizi kali, lakini Ndemla anashindwa kumalizia akiwa analitazama lango la Azam Dk 22, Kavumbagu anamjaribu Manyika, lakini anashindwa kulenga lango. MPIRA MAPUMZIKO: Dk 47, Simba ndiyo wanaonekana kuanza mashambulizi kwa kasi katika kipindi cha pili. Dk 54, Azam wanamtoa Kavumbagu wanamuingiza John Bocco GOOOOOOOO Dk 57, Azam FC anafunga bao la kusawazisha baada ya mabeki wa Simba kufanya uzembe. Anapiga shuti kali Dk 60, Okwi aanaumia, anatibiwa lakini inasindikana na inaelezwa amepoteza fahamu anaingizwa vyumbani akiwa amebabwa na madaktari. Dk 69, Simba wanamtoa Ndemla anaingia mkongwe shabaki Kisiga. Dk 65, Awadhi Juma anaingia kuchukua nafasi ya Okwi ambaye ameumia. Dk 72, mechi inaonekana kuchafuka na wachezaji wanachezeana kibabe, mwamuzi anamlaba kadi ya njano Mcha Ali Dk 78, Himid na Kessy wote wanalambwa kadi za njano kwa kuchezeana madhambi. Dk 79, Morris anapoga shuti kali sana lakini linatoka nje kidogo ya lango. Dk 82, Mcha anapiga shuti kali lakini Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa kabla ya mabeki kuondosha mpira. Dk 84 Azam wanafanya shambulizi kali lakini Manyika anafanya kazi ya ziada kuokoa. Dk 90+3 Simba wanapata kona nyingine Dk 90+2 Simba wanapata kona Dakika 4 za nyongeza MPIRA UMEKWISHAAAA
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: