i wish you happy chrismass and happy new year
Mbunge wa jimbo la Kahama (Picha kutoka Maktaba)
Wananchi wa Jimbo la Kahama mkoani Shinyanga wameaswa kuendelea na Kazi za uzalishaji mali na kuacha kukaa wakijadili masuala ya wagombea ubunge kwa kuwa wakati huo haujafika na wanaanzisha mijadala hiyo wanawatapeli watu.
Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo hilo James Lembeli kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Butibu Kata ya Kinamapula wilayani kahama ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake anayoifanya Jimboni humo.
Lembeli amesema kitendo cha watu kukaa kwenye makundi na kuanza kujadili wagombea kwa sasa ni kupoeteza muda kwa kuwa yeye bado anamkataba wa kuwatumikia wananchi hadi Agosti mwaka huu ndipo watakapoamua agomee tena au la.
Akifafanua juu ya ombi kla baadhi ya watu kutengeneza T-sheti za kuwagawia kama alivyofanya kamanda wa vijana weilayani humo Elias Kwandikwa Lembeli amesema, Kwandikwa kugawa T-sheti za kuwapendezesha vijana ni jukumu lake kama kamanda wao.
Lembeli amefafanua, yeye kama mbunge anayo kazi moja tu ya kupeleka maendeleo kwa wananchi, hivyo hawezi kuanza kuchapisha t-sheti huku wananchi wakichngishwa michango ya ujenzi wa shule, zahanati na maabara za shule.
Amesisitiza, kazi yake kama mbunge ni kuhakikisha anatafuta mbinu za kuwapunguzia mzigo wa michango hiyo wananchi kwa kutumia mfuko wa jimbo, wa kwake binafsi na wa wafadhili mbalimbali ili kuwaletea maendeleo.
Katika mkutano huo Lembeli amechangia shilingi 2,500,000= kwa ajili ya uakamilishaji jengo la zahanati huku akiadi kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la maji linalokikabili kijiji hicho
Katika kijiji cha Kasomela ambapo Ziara ilianzia kwenye katahiyo ya kinamapula, Lembeli amahidi kujenga nyumba ya mwalimu kuanzia boma hadi kupaua, baada ya kuambiwea kwamba, wananchi walikuwa wameshachangia boma likaangua baada ya ya halmashauri kushindwa kukamilisha.
Wakati huo huo Lembeli ameitaka Serikali ya Kijiji cha Butibu Kata ya Kinamapula wilayani Kahama kutoa taarifa ya matumizi ya Shilingi 3,000,000= zilizotolewa na mbunge wa jimbo la kahama James Lembeli kwa ajili ya matofari ya zahanati.
Lembeli ametoa agizo hilo kufuatia kusimama kwa jengo hilo huku pesa yote ya matofari ya kutosha boma alikuwa amekwisha itoa tangu mwaka 2008.
Lembeli amesikitika kuambiwa kwamba baadhi ya watu walikula hela hiyo ili kukwamisha mradi huo kwa lengo la kumshushia sifa aliyonayo ya kutekeleza ahadi za maendeleo na kutoa fursa kwa wagombea wengine wanaowania nafasi hiyo kuonekana wanafaa.
Awali lembeli amewambia wananchi kwamba wanatakiwa kuwa makini na wawaniaji wa uongozi wanaotumia pesa kuwahonga viongozi wa vyama ili kuwanadi na wengine kudanganya kugawia mabalozi wote baiskeli kwamba huo ni utapeli.
Amesema, pamoja na michezo hiyo michafu, siyo sahihi kutumia pesa iliyotolewa kwa maendeleo ya wananchi kwa nia ya kutafuta sifa ya kumwezesha mtu mwingine kupata uongozi hivyo atahakikisha watu walioshiriki wamekatwa na kushitakiwa.
Lembeli amefika kijijini hapo akiwa amepakia mabati 70 ya kuezekea zahanati hiyo akijua ilishakamika ujenzi wa Boma kabla ya kulazimika kurudi nayo na kwamba atapeleka mabati hayo mara tu ya boma kukamilika.
Na Marco Mipawa - Farajimfinanga.com - Kahama
0 comments:
Post a Comment