KWA KWELI HII NI KALI YA MWAKA, MAITI KUPASULIWA TUMBO NA KUZIKWA NA KUKU

i wish you happy chrismass and happy new year


henss
Katika hali isiyokua ya kawaida mwili wa Benadetha Steven mwenye miaka 35 aliyefariki dunia juzi umefanyiwa matambiko ya kimila baada ya kupasuliwa na wembe ukiwa kaburini na kuingizwa kuku ndani ya tumbo lake ikiwa ni ishara ya kuondoa mkosi.

Tukio hilo lilitokea juzi katika mtaa wa Mapinduzi, Shinyanga wakati waombolezaji wakiwa hatua ya mwisho ya kumzika marehemu lakini gafla alijitokeza ndugu wa marehemu mwanamke na kuwazuia waombolezaji huku mwenyewe akiingia kaburini  na kufungua sanduku kisha kumchana tumbo marehemu aliyekua akisumbuliwa muda mrefu na uvimbe tumboni.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema kaka wa marehemu ambaye hakutaka kujitambulisha jina lakini alikua kabila la Mkurya,aliupasua mwili wa marehemu kwa kutumia wembe kisha kuweka kifaranga cha kuku tumboni kikiwa hai na baadaye kufunika jeneza na kuruhusu maziko.

Walisema kabla ya tukio hilo kulitokea mabishano kati ya waombolezaji na ndugu wa marehemu wakitaka afanyiwe matambiko katika hospitali ya Mkoa wa Shinyanga alikokua akitibiwa.

“Mgogoro ulianzia nyumbani hata kabla ya kwenda makaburini,na wakati mazishi yanaendelea ndipo ndugu mmoja akaingia ndani ya kaburi akiwa amevaa mipira ya mikono ‘Gloves’ akiwa na wembe na boksi dogo lililokua na kifaranga cha kuku na kuzuia waombolezaji wasitupe udongo kaburini.

Inasemekana ndugu wa marehemu waliamua kufanya hivyo wakiamini wanaondoa mkosi ili kifo kama hicho kisitokee tena kwenye familia yao.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: