KIGOGO WA CHADEMA WILAYANI KAHAMA AKAMATWA NA NOTI BANDIA

i wish you happy chrismass and happy new year

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha

JESH la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga, linamshikilia kwa uchunguzi Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Sebastian Thobias maarufu kwa jina la "KOMAA" kwa tuhuma za kuhusika na mtandao wa noti bandia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema Thobias alikamatwa juzi na polisi wilayani Kahama kwa kuhusishwa na mtandao huo baada ya mwenzie kukamatwa na noti za bandia katika kata ya Kakola.

Kamugisha alisema tayari uchunguzi wa awali unaendelea kufanywa na polisi wa Kahama, ikiwa ni pamoja na kumfanyia upekuzi nyumbani kwake. Alisema baada ya uchunguzi huo kukamilika, watamfikisha mahakamani kujibu tuhuma hizo.

Kamanda huyo alisema kukamatwa kwa Thobias, ambaye pia ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Sazia katika Halmashauri ya Mji wa Kahama, kumetokana na kutajwa na mtuhumiwa Jonathan Denis (32), aliyekamatwa na Sh 750,000 za bandia huko Kakola.

“Tunamfanyia uchunguzi kwanza kujua mtandao wake, kama atabainika kuhusika na mtandao huo, sheria itachukua mkondo wake, hivyo sisi kama polisi lazima tufanye uchunguzi kabla hatujachukua hatua,” alisema Kamugisha.

Alisema Denis baada ya kukamatwa, alikutwa na vifaa mbalimbali, ikiwemo dawa ya kutengenezea noti hizo za bandia, na baada ya mahojiano na polisi alimtaja Thobias kuwa ndiyo mhusika mkubwa wa mtandao wa fedha za bandia Kanda ya Ziwa.


Kamugisha alisema tayari Denis ameshafikishwa mahakamani na Thobias kama atabainika, ataunganishwa na kesi hiyo. Alisema kwa sasa jeshi lake haliwezi kutoa ufafanuzi zaidi juu ya tuhuma hizo.

>>>Habarileo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: