Kamati ya Bunge Huduma za Jamii yatembelea Taasisi ya Mifupa, Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu(MOI)

Kamati ya Bunge na Huduma za Jamii imetembela Taasisi ya Tiba ya Mifupa , Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) ikiwa ni moja ya kufahamu shughuli mbalimbali zinazofanywa na wataalamu wa taasisi hiyo pamoja na kubaini changamoto mbalimbali zinazowakabili katika hutoaji wa huduma. Matembezi hayo yaliyoambatana na kikao cha kutafakali namna ya utoaji wa huduma na changamoto mbalimbali kimewashirikisha wadau mbalimbali wa afya akiwepo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dokta Seif Rashid kimeazimoa kuboresha zaidi miundombinu ya taasisi hiyo katika kutoa huduma zilizo bora kwa wananchi pasipo kuwa na uhitaji wa kwenda nje ya nchi kubata huduma hizo. Aidha kikao hicho kilifanya majumuisho ya mahitaji mbalimbali katika taasisi hiyo na hospitali kwa ujumla katika kuongeza tija ya kutoa huduma zenye ubora zaidi katika nyanja ya Tiba ya Mifupa ,Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu hospitalini hapo
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: