Msanii wa filamu za kibongo ambaye aliyewahi kuwa miss Tanzania 2006, ‘Wema Sepetu’ a.k.a ‘Madamu’ amefunguka kuwa anajuta kutumia kope za bandia kwa muda mrefu kwani zimeharibu kope zake za asili.
Wema alisema awali alikuwa hawezi kutoka kwenda kokote bila kuweka kope hizo na hata asipozibandika anajisikia vibaya lakini baada ya kumharibia muonekano wake wa asili, hataki hata kusikia.
“Jamani hakuna kitu ambacho nimekichukia kwa hivi sasa kama kope za bandia sina tena ushawishi nazo kabisa zimeharibu macho yangu, situmii tena,” alisema Wema
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment