i wish you happy chrismass and happy new year AZAM FC imelazimishwa sare ya kufungana mabao 2-2 na KCCA ya Uganda katika mchezo wa Kundi B, Kombe la Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Matokeo hayo, yanafanya timu zote za Kundi hilo zianze kwa pointi moja, baada ya mchezo wa awali baina ya Mtende FC na KMKM kumalizika kwa sare ya bila kufungana Amaan. Hadi mapumziko, tayari Azam FC walikuwa mbele kwao bao 1-0 lililofungwa na Nahodha wake, John Raphael Bocco dakika ya 38. Bocco alifunga bao lake la pili katika mechi mbili mfululizo alizocheza baada ya kuwa nje tangu Agosti mwaka huu maumivu, akimalizia krosi ya Mganda Brian Majwega. Awali alifunga katika sare ya 2-2 na Yanga SC mechi ya Ligi Kuu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: