FAIDA ZA ASALI

i wish you happy chrismass and happy new year


FAIDA ZA ASALI
Asali kama chakula na pia dawa ni dhana
kongwe katika historia ya mwanadamu. Kwa
mfano yapata miaka 4,000 (elfu nne)
iliyopita madakatari wa tiba wa Kimisri na
wale wa Sumarani waliitumia asali kutibu
magonjwa mbali mbali kama vile vidonda
vya tumnbo na vile vya kawaida, magonjwa
ya macho, ngozi na yale ya tumbo.
Historia pia imerikodi matumizi kama hayo
kwa watu wa Uchina, Ugiriki, Roma, n.k.
Hippocrates, baba wa tiba kwa nchi za
magharibi pia alitumia asali kutibu
magonjwa mbali mbali, vile vile Ibn Sina,
mfalme wa tiba kutoka katika ulimwengu wa
nchi za Kiislamu ameorodhesha faida nyingi
za matumizi ya asali, katika buku lake la tiba
maarufu "The Canon of Medicine". Miongoni
mwa faida alizotaja Ibn Sina katika buku hilo
(Misingi ya tiba) ni kuweka mwili katika hali
ya ujana, kuongeza uwezo wa kukumbuka
mambo, kuleta furaha, kusaidia usagaji wa
chakula kuongeza hamu ya kula chakula, na
kuongeza uwezo wa mtu kuzungumza vizuri.
Elimu ya Sayansi (ya kisasa) nayo
imemwezesha mwanadamu kufahamu kwa
kina ubora wa asali. Kwa mfano, tangu
mwaka 1937 wanasayansi walijua kwamba
wingi wa sukari iliyomo katika asali
(76gllooml), tindikali (acidity, Ph = 3.6-4.2),
na kuwemo kwa baadhi ya kemikali
zinazotokana na viumbe hai (Organic
Compounds). Ni sababu zinazoifanya asali
kuwa ni dawa. Yaani inaweza kuulinda mwili
usipate maradhi na pia inaweza kuviua
vijidudu vya maradhi vilivyomo ndani ya
mwili wa mgonjwa.
Zaidi ya hayo, sayansi inatujulisha kuwa,
asali inamchanganyiko wa virutubisho na
kemikali za aina mbali mbali. Baadhi ya vitu
hivyo ni sukari, vitamini, amino acids (vitu
vinavyotengeneza protini), vimeng'enyo
(enzymes), homeni (hormones).
(Sura ya 16, "An-Nahl"). Moja ya aya
inayopatikana katika sura hiyo
inayomwelezea kiumbe nyuki na teknolojia
yake kongwe ya utengenezaji wa asali ni hii:
(16:68).
Namalizia makala hii kwa kuwahimiza
wananchi wazidishe siyo tu uzalishaji bali
pia matumizi ya asali ili kujenga afya zetu
na uchumi wetu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: