CHADEMA YAMTAKA WAZIRI MUHONGO KUSITISHA ZIARA ZAKE ZA KISERIKALI

i wish you happy chrismass and happy new year


Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) kimemtaka waziri wa nishati na madini Mh.Prof.Sospeter Muhongo kuacha kuendelea kuwaongezea hasira watanzania kwa kutumia fedha za umma kufanya ziara za kiserikali, badala yake ajitathimini kama bado anazo sifa za kuendelea kuwa waziri baada ya kutakiwa kujiuzulu kutokana na kuhusishwa na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow.

Kauli hiyo imetolewa na naibu katibu mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalim wakati akihutubia mamia ya wakazi wa kisiwa cha ukara wilayani Ukerewe mkoani Mwanza ambako Chadema imefanikiwa kushinda vijiji saba kati ya vinane vinavyounda kisiwa hicho kutoka vijiji viwili ilivyokuwa navyo kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji uliofanyika desemba 14 mwaka jana, ambapo amehoji mapenzi ya Prof. Muhongo kwa watanzania kwa kuwaahidi umeme katika ziara yake ya mkoa wa mara huku akijua wananchi wanahasira na kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow ambako wizara yake ndio mhusika mkuu.
 
Aidha naibu katibu mkuu huyo wa Chadema Zanzibar Salum Mwalim, akihutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha nyamanga, kisiwani ukara amewataka watanzania kutorudi nyuma na badala yake waongeze umoja na mshikamano waliouonesha katika uchaguzi wa serikali za vijiji na mitaa ili kuing'oa CCM madarakani, huku mwenyekiti wa chama hicho wilayani Ukerewe Jacob Munyaga pamoja na mbunge wa jimbo la Ukerewe Salvatory Machemli wakieleza mikakati ya chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu.
 
Chama cha demokrasia na maendeleo ( Chadema ), kimeshinda vijiji 47 ,huku chama cha mapinduzi ( CCM ) kikishinda vijiji 27 na chama cha wananchi CUF kikishinda vijiji vitatu katika uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: