Breaking News Majambazi yavamia kituo cha Polisi, yaua polisi na kupora silaha

Kama Bado Hujajiunga Nasi, Unaweza Kujiunga Hapa Nikutumie Habari Moja Kwa Moja ..Bofya HAPA ULIKE PAGE YETU!.. Pwani, majambazi waliokuwa wamejihami, wakiwa na silaha wamevamia katika kituo cha Polisi cha Ikwiriri, Rufiji Mkoani Pwani ambapo inadaiwa wameua askari polisi wawili pamoja na kupora silaha zilizokuwemo katika kituo hicho. Aidha, tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo. Askari waliopoteza maisha ni Cop Edgar aliyafariki kwa kukatwa mapanga pamoja na Judith aliyepigwa risasi upande wa kushoto. Silaha zilizoporwa ni Smg 2, Sar2, Shortgun 1, silaha zingine pamoja na mabomu ya mchozi na takribani risasi 60 za bunduki aina ya SMG. Kwa mujibu wa mwananchi mmoja (jina limehifadhiwa) amesema kwamba leo asubuhi kuna makundi ya watu yamekusanyika katika eneo hilo ambapo jeshi la Polisi lipo katika harakati ya kusaka waliotenda tukio hilo. Mtandao wa Hivisasa utakujulisha zaidi kuhusiana na tukio hilo, endelea kuwa nasi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: