Afariki akicheza game siku tatu mfululizo

Mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Hsieh amefariki ndani ya internet cafe baada ya kupata ghafla tatizo la moyo, hiyo ni kutokana na ripoti ya Hospitali, camera za CCTV zinamuonyesha kuwa alikaa kucheza game hiyo kwa saa 72, sawa na siku tatu mfululizo. Michezo ya kwenye computer ambayo humpa nafasi mchezaji kucheza online ni maarufu sana Taiwan, watu wengi huipendelea kwa sababu ya unafuu wa gharama pia za mchezo huo. Wahudumu wa cafe hiyo wamesema ilikuwa kawaida ya Hsieh kucheza game kwa muda mrefu, akichoka huwa analaza kichwa kwenye meza hivyo hata wakati amefariki walihisi kwamba amelala kama kawaida yake.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: