WAZIRI KUCHANGIA TSH 15,000 MAAFA LUDEWA KWA FAIDA YA NANI?NI NANI AKUTOLEE ZAIDI ILI UKUBALI SIFA?


Jivunie kuwa mwana ludewa


ZIKIWA  zimepita  siku mbili  toka  uongozi  wa   serikali ya tarafa  ya Mawengi wilaya ya  Ludewa mkoani  Njombe   kuwapongeza  wadau mbali mbali   waliojitokeza  kuchagia shule ya  msingi Ludewa  mjini iliyokubwa na maafa  kwa  vyumba  vya madarasa  vitatu kuezuliwa na kimbunga na  uongozi  wa tarafa   hiyo  kuwashukuru  waliojitokeza  kuchangia akiwemo naibu  waziri  wa maendeleo ya jamii  jinsia na  watoto , Pindi Chana (mb) kiasi cha Tsh 15000 huku  waziri  huyo  aking’aka  kuchangia mchango  huu mtandao huu umekuja na ukweli zaidi ya mchango wa waziri  huyo.

Ifahamike  wazi kuwa  shule  hiyo  ilikumbwa na maafa  ya  kuezuliwa kwa paa  zake za  vyumba   hivyo  vitatu na hivyo  kupelekea  watoto  zaidi ya 200  kukosa  sehemu ya  kusomea na hivyo  kulazimika  kubanana katika  vyumba  vilivyopo toka Februari 28 mwaka  huu  maafa  hayo  yalipojitokeza.
 

Si mzazi  wala  mwalimu au  serikali ngazi ya  kijiji hadi Taifa  ambayo  ilipenda  kutokea kwa maafa  hayo  kwani  hilo lilikuwa ni  pigo  kubwa kwa  shule   hiyo na  njia  pekee ya  kutatua  tatizo  hilo  ilikuwa ni serikali  kupitia  kitengo  cha maafa ,Halmashauri ama  wadau  mbali  mbali  wakiwemo  wananchi na viongozi  wao kama madiwani na wabunge kwa maana  ya mbunge wa  jimbo na mbunge wa  viti maalum .

Katika  kuliona  hilo  waziri  Pindi ambae ni mbunge wa  viti maalum mkoa wa Njombe kupitia (CCM) alipata  kufika  shuleni  hapo May 5  mwaka  huu na  mbali ya  kuwapa  pore  walimu  kwa maafa  hayo mbali ya  zawadi  nyingine alizotoa  kwa    walimu  shuleni  hapo  ikiwemo ya  vitu  vya  kujisomea  wanafunzi pia  aliweza  kutoa zawadi ya kalamu  moja  moja kwa  walimu  wote  shuleni hapo tena  kwa  kuwafanya  walimu kukumbuka   zaidi alitoka  kalamu  zenye  nembo  ya  CCM na  zenye  jina lake Mh Pindi Chana  jambo ambalo si baya  ni  jema na linapaswa  kuungwa  mkono kwa  kila mdau  wa maendeleo ya  elimu katika kuwapa motisha   walimu wetu.
 

Mheshimiwa  waziri  wangu Chana ambae  ndie   wizara  yake  inahusika  na watoto kwa  kuliona  tatizo  hilo la  vyumba  vya madarasa  kuezuliwa alionyesha  kuguswa  zaidi na  hata  kuwa  kiongozi wa  kwanza  kuanza  kuchangia mchango kwa ajili ya harambee ya ujenzi  wa  vyumba  hivyo kwa  kuchangia kiasi  cha Tsh 15,000 kupitia kwa  mkuu  wa shule hiyo Agnes Mageza ambae  pia  kulingana na utaratibu  wa  ukusanyaji  wa fedha  hizo na  kuepuka matumizi yasiyo tarajiwa na  fedha  za  maafa  alilazimika  kufipeleka  fedha  hizo kwa afisa mtendaji wa  kijiji ili  kuzihifadhi  kwa taratibu  na kutoa stakabadhi kwa  kila mchangiaji kama  ambavyo taratibu  za  upokeaji  wa  fedha  za michago mbali mbali.

Pamoja na waziri  Pindi  mbunge wa Jimbo la Ludewa Deo  Filikunjombe katika kuunga mkono jitihada za  wapiga kura  wake  pia  kwa  wakati  huo alipeleka  saruji  mifuko 50  ili  kuanza  kukarabati  shule   hiyo huku  wananchi  wakichangishana  kiasi cha Tsh milioni 1.8 kati ya zaidi ya   Tsh milioni 13 zilizokuwa  zikihitajika ili kurejesha vyumba  hivyo  vya madarasa katika hali  yake na  watoto  wapata  kusoma.

Kasi  ya  michango kwa  wananchi ilikuwa chini   zaidi kwani hadi Desemba hii  ni Tsh milioni 1.8 pekee  na saruji  mifuko 50  ndio iliyopatikana  na kama kasi  hiyo ingeendelea  hivyo  basi  hadi  wananchi  hao  waweze  kujenga vyumba   hivyo kwa  kupata  Tsh milioni 13  basi ingekuwa ni mwakani mwezi Desemba.

Kwa  kuliona  hilo na uchungu  wa maendeleo ya  elimu kwa  watoto  hao mbunge Filikunjombe alilazimika  kujitolea  kujenga upya   vyumba hivyo kwa  zaidi ya Tsh milioni 13 ujenzi  ulioanza jumatatu wiki  hii na wakati wa  kujitole  kufanya   hivyo mkuu  wa  shule hiyo Bi Mageza na  katibu tarafa ya Mawengi   waliwashukuru  wadau  mbali mbali  waliochangia akiwemo waziri Chana aliyechagia Tsh 15,000 ila ajabu baada ya mtandao huu wa www.njenjenews.blogspot.com na mitandao  mingine na  vyombo  mbali mbali  vya habari  kuripoti  habari  hiyo ya waziri  kupongezwa kwa kuchangia kiasi hicho  cha pesa waziri Chana alinukuliwa akikana  kuchangia maafa katika  shule  hiyo na hata  kudai  kuwa Chadema wanamchafua .

Hivyo mtandao  huu wa  matukio umelazimika  kutafuta  ushahidi  wa kile  ambacho alikitoa pamoja na  wengine ambao  wamepata  kuchangia maafa  hayo kama  ukweli   huo unavyoonekana  hapo  juu.

Ushauri  wetu  kwa  mh Chana shule   hiyo  kuna majengo mengi ambayo yamechakaa hivyo si wakati  wa  kuanza  kuruka  kivuli  chako  mwenyewe  ni  wakati wa kuungana na mbunge mwenzako Filikunjombe kuleta maendeleo  kwa  wana Ludewa badala ya  kutafuta utukufu kwa msaada  usio na tija hivyo  kama umeona kiasi hicho  cha  fedha ni fedheha jitokeze  kuchangia zaidi ya ule ambao wengine  wamechangia  hata  kujitolea milioni 20 kwa ajili ya  kuboresha majengo ya  shule  hiyo.

Mwisho tunasema kamwe hatutakubali  kuwa manabii ya  uongo kukusingizia waziri Pindi  Chana kwa  jambo ambalo hujalifanya ili  tutaendelea   kukupongeza na  kukutia moyo  kuzidi  kuchangia kulingana na uwezo  wako japo  ukitoa padogo unapopongezwa usiruke  kivuli  chako.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: