Jivunie kuwa mwana ludewa
Wananchi wa kijiji cha Kitelewe wakishiriki kubeba bomba za maji zilizotolewa msaada na mbunge wao Filikunjombe |
Wannchi wa Kitewele wakimpokea mbunge Filikunjombe kushoto |
Baadhi ya wananchi wa kitewele wakiwakatika mkutano huo |
Wananchi wakimsikiliza mbunge wao kwa makini |
Mbunge
Filikunjombe kulia akijibu swali la mkazi wa kijiji cha Kitelewe
kushoto huku wakifurahi wote baada ya majibu mazuri ya kutaka wazee na
vijana kuungana kushiriki katika maendeleo
........................................................................................................
Na matukiodaimaBlog.
WANANCHI
wa Kijiji cha KITEWELE kata ya MAWENGI wilaya ya LUDEWA mkoani Njombe ,
wanatarajia kuanza kunufaika na huduma ya maji safi na salama ya bomba baada ya
kukamilika kwa ununuzi wa vifaa ikiwemo mabomba ya kutandika ardhini ambayo
yamegharimu kiasi shilingi zaidi ya Milioni 26
msaada uliotolewa na mbunge
wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe .
Akizungumza leo na wananchi hao mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo mbunge Filikunjombe alisema kuwa kukabidhi
kwa vifaa hivyo na mradi huo wa maji ni
utekelezaji wa ahadi yake ya maji kwa
wananchi hao aliyoitoa mwaka 2012 kufiatia ombi la
wananchi hao zaidi ya 800 waliokuwa
wakikabiliwa na adha ya maji .
Mbunge Filikunjombe alisema kuwa
toka nchi itape uhuru mwaka
1961 wananchi hao
hawajapata kuwa na maji safi
na salama na kuwa
miaka yote wamekuwa
wakitumia maji ya mito ambayo si
safi na salama kabla ya kufika na kuombwa
kuwasaidia kupata huduma hiyo ya
maji safi .
“Ndugu zangu nikiwa kama
mbunge wenu nimekuwa
nikiumia zaidi kuona
wananchi wangu mnapata
shida ya maji na ndio sababu ya
kuahidi kuungana nanyi katika kuwafikishia
huduma ya maji….ombi langu kwenu
tuzidi kushirikiana ili
kutatua kero zetu
bila kusubiri wahisani “
Miaka miwili iliyopita, Mbunge
wa Jimbo la Ludewa, DEO FILIKUNJOMBE alishuhudia kadhia hiyo akiwa katika
Zahanati ya kijiji hicho na akawaahidi wananchi kuwafikishia maji, ahadi ambayo
ameitekeleza mwaka huu na kukabidhi mabomba kwa wananchi yenye thamani ya zaidi
ya shilingi milioni 20 tayari kwa kuanza kazi ya kuchimba mitaro na kutandika
mabomba hayo.
Hata hivyo
alisema kuwa maendeleo ya
wananchi wa KItelewe na
jimbo la Ludewa
yataletwa na wananchi wenyewe
kwa kuunganisha nguvu
zao pasipo kusubiri wahisani na kuwa baadhi ya maeneo ya wilaya hiyo
wananchi siku zote
wamekuwa wakijitolea kushiriki katika maendeleo mbali
mbali.
Akielezea kuhusu adha ya maji katika jimbo lake na jinsi alivyoshiriki
kutatua alisema kuwa yapo maeneo ambayo wananchi wamekuwa na adha kubwa ya maji na tayari
ameanza kumaliza kero hiyo.
Kwa upande
wake diwani wa
viti maalum tarafa ya Mawengi Bilgeter Haule aliema kuwa moja ya
vitu ambavyo wana Ludewa
wanajivunia ni kumpata
mbunge ambaye anawajibika
kwa wananchi kama ilivyo kwa
mbunge huyo.
“
Tanzania mtu ambae hatakuj kusaulik ni pamoja na baba wa Taifa mwalimu Julius
Nyerere ambae alitanagazwa kuwa mwana heri ila kwetu Ludewa kutokana na kero tulizozipata
toka uhuru hadi
leo ambapo zinapatiwa ufumbuzi kwa pamoja tutamkumbuka mheshimiwa mbunge wetu
Deo Filikunjombe kama mwanaheri baada ya
kutatua kero zetu na kuondoka katika kundi la
watanzania wasiofurahia uhuru wao”
|
0 comments:
Post a Comment