WAUMINI WA KANISA ANGLIKAN IBUMI WILAYANI LUDEWA WAJENGA JENGO JIPYA LA KANISA

i wish you happy chrismass and happy new year


  


     Jengo jipya la kanisa Anglican Lililopo 
Na
Barnabas Njenjema ,Ludewa

Waumini wa kanisa Anglican Lililopo katika kijiji na kata ya ibumi wilayani ludewa katika mkoa wa njombe wameamua kushirikiana pamoja na kuanzisha ujenzi wa Jengo kubwa la kanisa kutokana na kanisa linalotumika kwa sasa kuwa dogo huku idadi ya waumini wanaoabudu katika kanisa hilo kuwa kubwa zaidi.


Wakizungumza Na mtandao huu hivi karibuni kijijini hapo waumini hao walisema kuwa wameamuakufanya hivyo kutokana na uwingi wa waumini wa kanisa Anglican kijijini hapo na kanisa linalotumika kwasasa ni dogo zaidi hivyo kujengwa kwa jengo jipya la kanisa hilo kutasaidia waumini wengi zaidi kuabudu katika kanisa hilo.

Walisema katika kuhakikisha kuwa jengo hilo linakamilika kwa muda muafaka waumini hao kwa pamoja waliamua kuchangia ujenzi huo kwa kufyatua tofali kwa kila jumuiya ya kanisa hilo na na kuchoma pia kuandaa kokoto, kuopoa mchanga pamoja na kutoa kiasi cha sh 40,000/= kwa kila muumini wa kanisa hilo.

Akifafanua malipo ya pesa hiyo muhudumu wa kanisa hilo bw, Michael Komba alisema kuwa pesa hiyo inatolewa kwa awamu nne ambapo kila awamu muumini atatoa kiasi cha sh 10,000/= na kuendelea mpaka kumalizika kwa mchango huo.

Hata hivyo muhudumu huyo alisema kuwa ujenzi huo ulianza rasmi miezi michache iliyopita kwa kukamilisha msingi wa mawe na mwezi November mwaka huu ujenzi wa jengo hilo ulianza rasmi hivyo waumini wa kanisa hilo wanaendelea kushirikiana na mafundi wanaojenga jengo hilo ililiweze kukamilika na kuanza kutumika.

Aliongeza kuwa jengo hilo litakamilishwa kwa hatua ya awali kwa kumwaga zege (bimu) eneo la juu litakapo ishia na baada ya hapo ujenzi huo utasimama na kuendelea kipiga paa na kuezeka bati mara baada ya mvua kusimama kwa msimu wa mwaka 2015.

Hata hivyo ujenzi wa jengo hilo unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo upungufu wa Bati, nondo, mifuko ya Saruji, nk hivyo waumini wa kanisa la Anglikan Ibumi wanawaomba wafadhili pamoja na wadau mbalimbali Tanzania kuwasaidia vifaa hivyo ili kuweza kukamilisha ujenzi huo.
Mwishoo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: