KIJANA BENNY WA KIJIJI CHA AMANI WILAYA YA LUDEWA ANAOMBA MSAADA WAWATANZANIA

i wish you happy chrismass and happy new year



BENNY Kijana ambaye ni mlemavu wa miguu

Hapa kijana BENNY amepiga magoti kutokana na ulemavu unaomkabili


Kijana benny ni mlemavu wa miguu tangu miaka mingi iliyopita kijana huyo anaishi katika kijiji cha amani kata ya mundindi katika wilaya ya ludewa mkoa wa njombe haliyake ni ngumu saana hasa katika suala la malazi na usafiri juu ya tatizo lake kwakuwa mpaka sasa mlemavu huyo hana wazazi kutokana na wazazi wake wote wawili kutangulia mbele ya haki.

Mlemavu huyo anatembea kwa kutambaa ili kufika kila semu anakohitaji kufika kutokana na halingumu aliyokuwanayo hivyo inamlazimu kufanya hivyo licha ya kuwa anateseka saana hasa kwa kutumia mikono yake miwili kama miguu.


Hata hivyo kijana huyo hanauwezo wa kuzungumza maneno ya kueleweka anazungumza kwa shida saana wakati mwingine hulazimika kukaa karibu na mtu au kitu anacho kihitaji iliawezekupata msaada.

Mmiliki wa mtandao huu Bw, Maiko luoga aliweza kufika katika kijiji hicho na kukutana na kijana huyo hivyo kujionea halihalisi juu ya maisha ya mateso anayopata mlemavu huyo na kufanya uamuzi wa kuzisambaza habari hizi katika mitandao ya kijamii ili kijana huyo aweze kusaidiwa.

Kwasasa kijana huyo anatunzwa na wajomba zake ndio ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa kijana huyo hivyo wajomba zake walisema kuwa kama kijana wao angepata msaada wa aina yoyote ingekuwa msaada mkubwa saana kwa kijana benny.

Hata hivyo kwa yeyote aliyeguswa na kijana huyo anaweza kuwasiliana na mtandao huu kupitia namba za simu 07 6270 5839/ 06 5560 5839 ili kuweza kumsaidia kijana huyu.


Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: