WANANCHI WACHANA BENDERA YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM KATA MLANGALI WILAYANI LUDEWA
Chama cha mapinduzi CCM wilayani ludewa Mkoa wa Njombe kinaendelea na mchakato wa kuwatafuta watu wote waliojihusisha na vitendo viovu ikiwemo Kampeni za matusi na kuchana bendera za chama hicho katika eneo la kata ya Mlangali ili kuweza kuwatia mbaroni wale wote walio jihusisha ikiwemo kufikishwa mahakamani katika kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa na hatimaye kuwekwa ndani mpaka uchaguzi huo utakapoisha.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Desember 8 mwaka huu katika eneo la soko kuu la Kata ya mlangali na kuhudhuriwa na wanachama pamoja na viongozi mbalimbali ngazi ya taifa akiwemo Naibu katibu mkuu wa umoja wa wazazi Tanzania bw, Groriasy Luoga pamoja na wajumbe wa kamati ya utekelezaji ngazi ya mkoa, Katibu wa Chama cha mapinduzi CCM wilaya ya ludewa katika mkoa wa njombe Bw, Elwudi Shemauya Alisema kuwa kuna baadhi ya wananchi wanao dhaniwa kuwa ni wavyama pinzani waliamua kuchana bendera hizo za CCM katika kata ya mlangali kwa lengo la kukishusha chama hicho kisipite katika uchaguzi wa serikali za mitaa.
Alisema Wahusika wa vitendo hivyo lazima wapatikane na kuchukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kifungo ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo visiendelee hasa katika kampeni za vyama mbalimbali vya siasa zinazoendelea kufanyika hivi sasa katika kuelekea tarehe ya uchaguzi Desember 14 mwaka huu na kuongeza kuwa licha ya vitendo hivyo chama hicho kimepokea taarifa ya matusi kutoka vyama vya upinzani wakati vyama hivyo vinapo kuwa katika kampeni zake vitendo ambavyo si sawa na vitendo hivyo vilisha zuiwa na msimamizi wa uchaguzi wa serikali za mitaa wilaya na taifa kwa ujumla.
Alisema kila chama ni lazima kisimamie sharia zake bila kuathiri uhuru wa chama kingine kwa lengo la kuleta maendeleo katika taifa la Tanzania kwakuwa kwa kuweka malumbano hakuna maendeleo yatakayo patikana hivyo wananchi nilazima wajue baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wanapenda kuzungumza mabaya ya ccm bila kujua ni mambo mangapi makumbwa na mazuri ambayo chama cha mapinduzi kimefanya badala yake wanawachanganya wananchi kwa kusema kuwa wasikichague chama hicho hali ambayo si kweli.
Kwa upande wake Katibu wa umoja wawazazi wilaya ya ludewa Bi, Daima Nyoni alisema kuwa wananchi wa wilaya ya ludewa ni lazima watambue kuwa chama cha CCM ndicdo chenye mamlaka ya kuiongoza nchi ya Tanzania hivyo wananchi hawapaswi kuhangaika nilazima watulie na chama chao wakiendelea kukichagua ili kizidi kuongoza nnchi kwa manufaa ya kila mtanzania.
Katibu wa umoja wa wazazi wa CCM wilaya ya Ludewa Bi, Daima Nyoni
Bi, Daima Nyoni Katibu wa umoja wa wazazi wilaya ya Ludewa
Hata hivyo aliongeza kuwa kwasasa wilaya ya ludewa na taifa la Tanzania kwa ujumla lipo katika mchakato wa kuwapata viongozi wa serikali za mitaa hivyo wapiga kura wasibabaishwe nilazima watambuae chama kinacho wasaidia katika maisha yao ya kila siku ndio chaguo lao haina haja ya kukikataa chama kwa changamoto chache ambazo kinacho chama kwakuwa changamoto hizo zinauwezekano mkubwa wa kutatuliwa.
Aliwataka wanachama na wananchi wote wilayani ludewa kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 14 katika uchaguzi huo ili kuweza kupata nafasi ya kuwachagua viongozi wanao wafaa kuwaongoza wananchi hao
0 comments:
Post a Comment