AJALI YATOKEA KATIKA BARABARA KUU YA LUDEWA NJOMBE
Ajali hiyo imetokea mapema desember 8 mwaka huu majira ya saa mbili asubuhi jirani na kijiji cha mbwila katika kata ya luana barabara kuu ya ludewa / Njombe na kuhusisha gari lenye namba za usajiri T 379CXT Costa Collina mali ya Kampuni ya Mosses Express linalo jihusisha na kusafirisha abiria kutoka ludewa mjini na kuelekea njombe mjini na gari lenye namba za usajiri T 722BGJ Tipa aina ya Fuso linalofanya kazi ya kubeba kifusi kwaajiri ya kuboresha barabara hiyo.
Kwa mujibu wa mashuhuda walio shuhudia ajali hiyo ambao walikuwa wanasafiri kutoka Ludewa kuelekea njombe walisema kuwa ajali hiyo ilisababishwa na kona kali pamoja na vifusi vilivyo wekwa barabarani humo kwaajiri ya maboresho ya barabara hiyo bila kusambazwa hivyo kuifanya baraba hiyo kuwa nyembamba zaidi haliiliyo sababisha dereva wa basi kushindwa kuona mbele na kasha kuanza kukata kona kwa haraka ili kukwepa gari lililo kuwa mbele bila mafanikio nakusababisha ajali hiyo.
Walisema gari hilo linalojihusisha na ukarabati wa barabara lilikuwa likitokea mbwila kuelekea ludewa wakati basi walilokuwa wanasafiria abiria hao lilikuwa likitoka ludewa kuelekea njombe hivyo magari hayo yaligongana maeneo ya ubavuni na kisha kusababisha gari aina ya Costa kuvinjika katika eneo la kioo kikubwa cha nyuma pamoja na ubavu wa kulia liliko bamizwa, wakati fuso hilo likitoka salama bila kuvunjika.
Mmiliki wa mtandao huu aliweza kufika katika eneo la tukio na kujionea halihalisi ya ajali hiyo jinsi ilivyoweza kutokea na kubaini kuwa katika ajali hiyo hakuna mtu/watu waliopoteza maisha na baada ya kuzungumza na abiria hao juu ya usalama wao aligunduliwa kijana mmoja ambae hakuweza kufahamika jina wala makazi yake maramoja kuwa amejeruhiwa sehemu yake ya mkono wa kulia na kumsababishia maumivu na ndipo wasamalia wema walimkimbiza majeruhi huyo katika zahanati ya kijiji cha mbwila kwa kupata huduma ya kwanza ilikuendelea na matibabu.
Kijana aliye jeruhiwa katika ajali hiyo
Hata hivyo mwandishi wetu mpaka anaondoka katika eneo la tukio aliwaacha askari wa usalama barabarani wakiwa wamefika katika eneo hilo wakiwa wanaendelea na uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini chanzo cha ajali hiyo, huku wahusika wa magari hayo wakiwa katika hatua za kuweza kuwafaulisha abiria wanao elekea njombe ili waweze kuendelea na safari.
Askari wa Usalama Barabarani wakikagua eneo la ajali
Na maiko luoga, ludewa Tazama jinsi ajali hiyo ilivyo tokea
Mosses Express
Na wananchi wa vijiji vya mbwila na luana wilayani ludewa wamewataka madereva wa vyombo vya moto kuwa makini mara wanapo kuwa barabarani ilikuweza kuepuka ajali zinazoweza kuepukika.
0 comments:
Post a Comment