UTABIRI WA MAALIM HASSAN YAHYA WAMPA DR HAMISI KIGWANGALLAH URAIS 2015

Akitabiri juu ya urais na sifa, Alisema mwenye sifa hizo, ndiye atakayekuwa Rais pekee mwenye nyota ya kudumisha sifa ya Tanzania ya amani na utulivu kwa kuwa mwaka 2015, utaanza siku ya Alhamisi, ambayo kinyota hutawaliwa na sayari ya Mushtara (Jupiter) yenye nyota za Mshale na Samaki. Maalim Hassan alisema Rais pekee mwenye nyota hiyo, ana sifa ya kuwa kijana mwenye mchanganyiko wa dini mbili za wazazi na/au ndoa zadini tofauti. Hata hivyo, baadhi ya waandishi wa habari walimweleza Maalim Hassan kuwa sifa hizo zinamlenga moja kwa moja January Makamba, hivyo wakataka kujua sababu za nyota kutokutaja kabisa jina la kiongozi huyo. Akijibu swali hilo, Maalim Hassan alisema yeye hajui watu wote waliotangaza azma ya kutaka kugombea urais. Alisema zaidi ya hivyo, miongoni mwa aliowasikia wakitangaza yumo pia Hamisi Andrea Kigwangallah, Mbunge wa Nzega (CCM), ambaye majina yake yanaonyesha kuwa yanatokana na dini tofauti. Ingawa maalim Hassan alimtaja Dr Hamisi Andrea Kigwangallah lakini January Makamba, ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli (CCM) ni kijana mwenye umri wa miaka 41, ana mchanganyiko wa dini mbili za wazazi.Baba yake mzazi, Yusufu Rajab Makamba ni muislamu na mama yake mzazi, Josephine ni Mkristo wa madhehebu ya Katoliki. Wajuzi wa mambo ya siasa wanasema utabiri wa maalim Hassan unaweza kwenda kombo labda hao anaowatabiria wajienguwe kutoka chama tawala kutokana na hali ya hewa ya escrow na serikali tatu
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: