UMEIPATA HII......Laveda Arudi tena Big Brother Africa

Mwanadada aliyewakilisha Tanzania katika shindano la BIG BROTHER 2014 ‘HOTSHOTS’ nchini Afrika Kusini. Irene Neema Vedastous 'La Veda' ameitwa tena ili kushuhudia fainali za kinyang’anyiro hicho. Mrembo huyo amepanda pipa juzi saa 8 mchana kuelekea Sauz ambapo atakaa kwa muda wa wiki moja. Akizungumza na mwandishi wetu, La Veda alisema ameitwa Sauz japo bado hajajua anaenda kufanya nini hasa japo anaamini hataingia kwenye jumba la BBA kama mshiriki. ‘’Nimeitwa BBA ila si kwa maana ya kushiriki bali kama mmoja wa washiriki ili kushuhudia fainali za BBA zinazotegemea kufanyika hivi karibuni. "Ninafurahi kwa sababu nitakutana na washiriki wenzangu, kama nikibahatika kupata nafasi ya kuimba, wimbo wangu mpya wa LET IT GO, nitafanya makubwa sana maana muda mwingi na akili yangu nimeviwekeza kwenye muziki, nitakuwa Sauz kwa wiki moja kisha nitarejea nyumbani kujipanga zaidi kimuziki"Alisema La Veda. Aidha La Veda amemtakia kila la heri mshiriki mwenzie Idris Sultan ashinde na amewaomba Watanzania kumuombea kwani ushindi wake ni ushindi wa Watanzania wote.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: