Uchaguzi wa Serikali za Mitaa waingia Dosari

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji uliofanyika jana nchini Tanzania ulitawaliwa na kasoro na vurugu zilizosababisha polisi kutumia risasi na mabomu ya machozi huku baadhi ya wapiga kura wakipigana sehemu tofauti tofauti nchini. Vurugu hizo zilitokana na uchaguzi huo kugubikwa na kasoro nyingi na hivyo kusababisha baadhi ya vituo kulazimika kuahirisha uchaguzi hadi wiki ijayo. Vurugu hizo ziliripotiwa katika mkoa wa Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza, Kigoma, huku kasoro hizo zikitajwa kuwa ni baadhi ya vituo kuchanganya majina ya wagombea , kuchelewa kuanza kwa uchaguzi, kukosekana kwa vifaa vya kupigia kura na Mengineyo. Katika Vurugu zilizojitokeza Jijini Dar es Salaam Jeshi la Polisi Wilaya ya Kinondoni linawashikiliwa watu kadhaa kwa mahojiano zaidi.Hali ilikuwa sana katika Mtaa wa Kazima uliopo Kinondoni, baada ya uchaguzi kushindwa kufanyika kabisa, kufuatia vurugu zilizosababisha msimamizi wa uchaguzi katika kituo hicho kuhairisha uchaguzi huo. Wakati mikoa hiyo ikitawaliwa na vurugu hizo, mamia ya wananchi wa maeneo mbalimbali mkoani arusha walijitokeza kupiga kura kwa amani na utulivu hali iliyoashiria baadhi ya wananchi kuaanza kupata uelewa wa masuala ya kisiasa na kutambua haki zao. Na katika matokeo ya awali kwa baadhi ya mikoa imeonyesha kwa sehemu kubwa ya uongozi umeangukiwa mikononi mwa vyama vya upinzani.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: