Takwimu mbaya kwa Arsenal
Hali ndani ya klabu ya Arsenal imezidi kuwa mbaya baada ya mashabikiw a klabu hiyo kuendelea kushinikiza kuondoka kwa kocha wao Arsene Wenger . Shinikizo hilo liliongezeka mwishoni wa wiki iliyopita wakati Arsenal ilipofungwa na Stoke City kwa matokeo ya 3-2 kwenye uwanja wa Brittania .
Mashabiki wa Arsenal baada ya mchezo huo walichapana Makonde baada ya kutokea mabishano makubwa baina ya makundi mawili ambayo mojawapo lilikuwa linaunga mkono Wenger Kuondoka huku lingine likimtaka kocha huyo aendelee kubaki madarakani.
Takwimu zinazidi kuwapa sauti wale wanaotaka Wenger aondoke ambapo imefahamika kuwa Arsenal imekuwa ikifungwa baada ya wapinzani wake kupiga shuti la kwanza lililolenga shabaha ya lango katika michezo takribani saba kati ya 15 ambayo Arsenal imecheza. Hadi sasa Arsenal ambayo iko kwenye nafasi ya tano ambaimekusanya pointi 23 baada ya michezo 15 huku ikiwa imeshinda michezo 6 pekee , ikitoka sare kwenye michezo mitano na kupoteza michezo sita .
Arsenal imefungwa mabao saba yaliyotokana na shuti la kwanza katika michezo saba kati ya 15 ya ligi ya England.
Mabingwa hawa wa kombe la FA wataingia uwanjani hapo kesho kutafuta tiketi ya kufuzu hatua ya 16 kama washindi wa kundi lake watakapokuwa wanacheza na Galatasaray ya Uturuki.
0 comments:
Post a Comment