SIMBA YAMALIZANA NA BEKI KISIKI WA GOR MAHIA, HANS POPPE AMZUNGUMZIA
Simba imemalizana na beki David Owino wa Gor Mahia.
Uongozi wa Simba kupitia kamati yake ya usajili, imefanya mazungumzo na beki huyo na kumalizana naye, kilichobaki ni suala la kuanguka saini tu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hans Poppe amesema wanachosubiri ni kumuona na kumalizana naye katika usajili.
"Kweli mazungumzo yamekwenda vizuri na Gor Mahia pia wamekubali, suala ni kukutana naye na kujua nini cha kufanya," alisema Hans Poppe.
0 comments:
Post a Comment