BURUNDI WALITIA MCHANGA PILAU LA UHURU, WAICHAPA 2-1 STARS MABORESHO TAIFA

KIKOSI cha pili cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, maarufu kama ‘Taifa Stars Maboresho’ jioni hii kimefungwa mabao 2-1 na Burundi katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Katika mechi hiyo maalum iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kusherehekea miaka 53 ya Uhuru, Stars Maboresho ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 11 kupitia kwa Yussuf Rashid. Burundi walichangamka baada ya bao hilo na kuanza kusukuma mashambulizi ya nguvu langoni mwa Maboresho iliyoongozwa na Kocha Mkuu wa Tanzania, Mholanzi Mart Nooij. Mshambuliaji wa Tanzania, Atupele Green akiwa amekaa chini huku Abbas Nshimirimana wa Burundi akiufuata mpira Kwa kutumia vyema udhaifu wa safu ya kiungo ya Tanzania, Burundi walitawala mchezo na kufanikiwa na kupata bao la kusawazisha dakika ya 25, mfungaji Fabrice Mimimahazwe kabla ya kupata bao la ushindi dakika ya 72 kupitia kwa Nassor Niyonkuru. Maboresho walicharuka baada ya kufungwa bao la pili na kuanza kushambulia mfululizo, lakini kipa wa Burundi, Innocent Mbonihankuye alikuwa kikwazo kwao kupata bao. Kwa ujumla, Stars Maboresho haikucheza soka ya kuvutia na maana yake Mart Nooij ana kazi kubwa ya kufanya kuiboresha timu hiyo.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: