SERIKALI KUPITIA REA YATOA SHILINGI MILIONI 150 KWAAJILI YA UMEME VIJIJI 19 WILAYANI LUDEWA.

Jivunie kuwa mwana ludewa


 Maporomoko ya mto Lupali
Msitu wa mto Lupali



Serikali kupitia Wakala wa umeme vijijini nchini (REA) imetoa kiasi cha shilingi 150 milioni ili kufanikisha mchakato mzima wa upembuzi yakinifu katika vijiji 19  wilayani Ludewa katika mkoa wa Njombe, umeme ambao utazalishwa katika mporomoko ya mto Lupali katika kijiji cha Njelela kata ya Mundindi na kusimamiwa na shirika lisilo la kiserikali la Ludewa Capacity Bulding Asosiation(LCBA).

Umeme huo ambao utazinufaisha kata 6 zenye vijiji 19 tayari kazi ya upembuzi yakinifu imekwisha anza na unatarajiwa kuzalishwa megawati 10 ambazo zitasambazwa katika vijiji hivyo na unaobaki unatarajiwa kuuzwa katika shirika la Tanesco kutokana na umeme huo kuwa mwingi kuliko idadi ya watumiaji.

Akiongea katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Amani kata ya Mundindi Mwenyekiti wa shirika la LCBA Bw,Visent Magombola alisema kazi ya kujenga mitambi ya kuzalishia umeme na kuusambaza kwa jamii inatarajia kuisha ndani ya mwaka mmoja na nusu hivyo wananchi wanatakiwa kujiandaa kwa kujenga nyumba bora.

Bw.Magombola alizitaja kata na vijiji vyake ambavyo vinatarajia kunufaika na nishati hiyo kuwa ni Kata ya Mkongobaki katika vijiji vya Lipangala,Ugera na Mkongobaki,Kata ya Lugarawa katika vijiji vya Mdilidili na Shaurimoyo,kata ya Mundindi ni vijiji vya Amani,Mundindi na Njelela,kata ya Ibumi ni vijiji vya Ibumi na Masi mavalafu.

Nyingine ni kata ya Madilu katika vijiji vya Ilawa,Ilininda,Madilu,Manga na Mfalasi,Kata ya Madope ni vijiji vya Luvuyo,Madope,Lusitu na Mangalanyene hivyo wataalamu wa upembuzi yakinifu tayari wako kazini ili kuiwahisha ripoti ambayo itasaidia ujenzi wa mashine za kuzalisha umeme kuanza mapema.

“Serikali kupitia wakala wa nishati ya umeme vijijini REA wametupatia fedha kiasi cha shilingi 150 milioni kwaajili ya mchakato wa upembuzi yakinifu katika vijiji 19 ambao kupitia wataalamu tayari hatua mbili tumeshazifanya bado moja ya mwisho ambayo itakamilisha ripoti ya kuanza kazi rasmi hivyo wananchi mnatakiwa kujiandaa kwaajili ya ujio wa umeme huo kupitia maporomoko ya mto Lupali katika kijiji cha Njelela”,alisema Bw.Magombola.

Bw.Magombola alisema kumekuwa na uvumi mkubwa na kashfa nyingi kutoka katika mashirika mbalimbali yakidai LCBA haina uwezo wa kupata pesa za kuanzishia mradi huo,hali ambayo sio kweli kutokana na shirika lake kuaminiwa na Serikali kwa kiwango kikubwa ambacho mpaka sasa tayari fedha zimeshatolewa kwaajili ya kazi hiyo.

Aliwataka wananchi kutojibweteka kwani kuna fulsa nyingi za uwekezaji kama uanzishwaji wa viwanda vidogo vigodo ambavyo vitaweza kupunguza hali ya umaskini ambayo imekithiri vijijini kwani umeme huo ni mkubwa tofauti na mashirika yote yanayozalisha umeme wilayani Ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: