ROONEY APIGA MBILI, AMSETIA VAN PERSIE MAN UNITED IKISHINDA 3-1

MANCHESTER United imeendelea kufanya vizuri katika Ligi Kuu ya England kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Newcastle Uwanja wa Old Trafford. Ilikuwa ni siku nzuri kwa Nahodha Wayne Rooney, aliyeifungia Manchester United mabao mawili na kutoa pasi ya bao moja, la tatu. Rooney alifunga bao la kwanza kwa pasi ya Radamel Falcao dakika ya 23 katika shambulizi alilolianzisha mwenyewe kutokea nyuma, kabla ya kufunga la pili dakika 13 baadaye kwa pasi la Juan Mata. Nahodha huyo wa England pia, akampasia mpira mzuri Robin van Persie kufunga bao la tatu kwa kichwa dakika ya 53, kabla ya Papis Cisse kuifungia bao la kufutia machozi Newcastle kwa penalti dakika ya 87. Kwa ushindi huo, Mashetani Wekundu wanaendelea kukamata nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu, wakizidiwa pointi 10 na vinara, Chelsea Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Jones, McNair, Evans, Valencia/Rafael dk80, Rooney, Carrick/Fletcher dk62, Young, Mata, Falcao/Wilson dk65 na Van Persie. Newcastle: Alnwick, Janmaat, Steven Taylor, Coloccini, Dummett/Cabella dk63, Anita, Colback, Armstrong/Cisse dk63, Sissoko, Gouffran na Perez/Vuckic dk82.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: